- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
MAHITAJI: Unatakiwa kuwa na:
Ø Chumba maalumu kisichopitisha mwanga
Ø Presure cooker au jiko maalumu lenye moto mkali
Ø Vyombo vya kuwekea mbegu kama vile glass
Ø Maji salama
Ø Ungaunga wa viazi vitamu
Ø Uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu
Ø Kibakuli kidogo chenye mfuniko na
Ø Kipande cha uyoga (ambacho kitachanganywa na maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu, kwa ajili ya kutengeneza fangasi ambao watatumika kutengeneza mbegu ya uyoga)
HATUA YA KWANZA: Kuandaa fangasi
1. Changanya kipande cha uyoga na maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu, kwa ajili ya kutengeneza fangasi ambao watatumika kutengeneza mbegu ya uyoga)
2. Baada ya kuchanganya mchangnyiko huo, chemsha mchanganyiko huo kwenye presha cooker au jiko la moto mkali.
3. Ipua na weka mchanganyiko huo kwenye vibakuli vidogo vinne vyenye mfuniko
4. Acha upoe kwa dakika kumi na tano.
5. Chukua vipande vya uyoga weka kwenye mchanganyiko uliouweka kwenye bakuli ndogo yenye mfuniko halafu funika na hifadhi katika sehemu yenye joto (room temperature) ili kukuza fangasi kwa muda wa siku kumi au kumi na tano.
6. Baaada ya siku kumi na tano fangasi zitakuwa tayari kwa ajili ya kuendelea kuandaa mbegu ya uyoga.
7. Hifadhi fangasi hao kwenye friji ili wasiendelee kukua.
HATUA YA PILI: Kuandaa mbegu za uyoga
Baada ya kuandaa fangasi hatua inayofuata sasa ni kuandaa mbegu ya uyoga, fuata hatua zifuatazo:
1. Andaa mtama kilo hamsini [kg 50]
2. Chemsha mtama kwenye jiko lolote mpaka uive kwa kupasukapasuka
3. Ipua na chuja maji
4. Baada ya kuchuja weka mtama wako kwenye chupa au kopo lenye mfuniko, weka katika chupa nyingi kadiri uwezavyo.
5. Weka kwenye preasure cooker au jiko lenye moto mkali kwa muda was aa moja
6. Ipua na acha upoe
7. Baada ya kupoa chukua fangasi katakata vipande vipande na kila kipande weka kwenye kopo au chupa yenye mtama.
8. Funika kwa muda wa siku kumi na tano mbegu itakuwa imekomaa na tayari kwa kupandwa katika shamba uliloliandaa.
Aina ya mbegu tuliyoiandaa hapa ni mamama (oyster mushroom). Uyoga ni zao linalotumika kukuza uchumi kwa wakulima kwani linahitajika sana mahotelini kwa ajili ya supu. Lakini uyoga huo pia unatumika majumbani kwa mlo ambao una lishe bora kwa familia.
Soma: Namna ya kuzalisha uyoga
NB: Mahitaji yote unaweza kuyatengeneza ukiwa nyumbani au unaweza kuyapata kwa kununua kwenye maduka kwa kutumia majina yafuatayo;
- Auger - ungaunga wa viazi vitamu
- Distilled water - maji salama
- Beaker - glass
- Malt extract - uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitam
- Petri dishes - kibakuli kidogo chenye mfuniko
- Distilled water - maji salama
- Beaker - glass
- Malt extract - uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitam
- Petri dishes - kibakuli kidogo chenye mfuniko
Comments
Post a Comment