- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
MUHTASARI
Ugonjwa wa Mnyauko bakteria wa migomba (Banana Xanthomonas Wilt, BXW) umepewa jina lake kutoka kwa bakteria wanaoambukiza na hatimaye kuua mgomba. Ugonjwa huo umeongezeka sana nchini Tanzania tangu ulipogundulika kwa mara ya kwanza mwaka wa 2006 mkoani Kagera ukutokea nchini Uganda.
Aina zote za migomba hushambuliwa ingawa matokeo ya utafiti yameonyesha uwezekano wa kupatikana kwa aina sugu siku zijazo. Aina kuu ya usimamiaji kwa sasa ni kuzingatia usafi wa shamba: kupanda mazao ya afya, kutumia zana safi za kukatia na kuondoa maua dume ili kupunguza kuathiriwa kupitia wadudu wanaobeba bakteria wakati wanapofyonza utomvu.
VISABABISHI
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria Xanthomonas campestris pv. musacearum. ‘pv.’ husimamia kwa neno pathovar na inaonyesha aina fulani ya X. campestris ambayo huambukiza tu migomba pekee na jamii yake ya karibu ya ensete. Hapo awali ilikuwa inajulikana kama X. musacearum. Bakteria wanaweza kuenea kwa njia ya wadudu wanaotembelea maua ya mimea iliyoambukizwa na kisha kulisha juu ya mimea safi na pia kupitia njia ya zana zakukata zilizo na bakteria.
Kimataifa, kuna aina kadhaa za mnyauko bakteria ambazo husababisha dalili sawa na pia kuishi katika njia sawa kama BXW. Nyauko hizi zinahusishwa na aina tofauti ya bakteria Ralstonia solanacearum, ambayo haishambulii migomba katika Afrika.
Mwaka 2003 utafiti ulianza kufanyika nchini Tanzania Mkoani Kagera ili kubaini kama ugonjwa huo umeshaenea ,ambapo haukugundulika mpaka kufikia mwaka 2006 Januari uligundulika katika kijiji cha Kabale kilichopo tarafa ya Izigo wilaya ya Muleba.
Mnamo Januari mwaka 2006 hadi juni 2012 ugojwa wa unyanjano ulikuwa umeenea wilaya mbalimbali za mkoa huo, isipokuwa wilaya ya Biharamulo huku jumla ya kata 110,vijiji 389 na kaya 56,520 zikiripotiwa kuathirika na ugonjwa huo. Maeneo mengingine ya Tanzania Ugojwa ulithibitishwa ni pamoja na wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Chato na Geita katika Mkoa wa Geita ,kasulu,Kibondo,na Kakonko Mkoa wa Kigoma pamoja na wilaya ya Ukelewe Mwanza.
DALILI MUHIMU
Alama kubwa zaidi ya ugonjwa wa BXW ni kuwa ndizi huiva mapema kabla ya kukomaa: Vidole kadhaa huanza kuwa na rangi ya manjano na vyengine kwenye mkungu kubakia rangi ya kijani. Vikikatwa, vidole huwa na rangi nyeusi hata pamoja na vile ambavyo ni rangi ya kijani. Vidole huwa vyeusi kwa haraka na hatimaye mkungu wote huoza.
![]() |
Ndizi iliyoharibiwa na BXW |
Ishara ya kwanza ya maambukizi, hata hivyo, ni wakati majani ya rangi ya zambarau ya maua ya kiume hunyauka, kuwa meusi na kufa. Pia angalia majani machanga sehemu ya juu ambayo hugeuka rangi ya manjano, kukunjika katikati na kisha kuanguka. Kata shina la mkungu, na utomvu unapoisha kutoka angalia madoa madogo ya rangi ya manjano. Haya yanaonyesha kwamba bakteria wanazuia mtiririko wa maji na virutubishi. Hata hivyo, inawezekana kuwa vigumu kuona madoa haya madogo ya rangi ya manjano.
![]() |
Shina la mgomba lenye ugonjwa wa BXW |
Ugonjwa wa kuvu wa migomba, unaojulikana kama Fusarium wilt au ugonjwa wa Panama, pia husababisha rangi ya manjano lakini kwenye majani yaliyozeeka. Jani halijikunji na manjano yake ni kali zaidi ikilinganishwa na BXW. Matunda huendelea kawaida. Dalili ya kutofautisha Fusarium wilt ni rangi nyeusi ndani ya shina, ambayo haiko kwenye migomba iliyoambukizwa na mnyauko bakteria.
ATHARI
BXW ni ugonjwa mharibifu sana unaoathiri kila aina ya migomba. Mimea na matunda huharibiwa. Ugonjwa unaweza kuenezwa mbali kwa njia ya vipandikizi na mabaki ya mimea. Haja kubwa ya ndizi katika Kampala huvutia kuletwa kwa bidhaa kutoka mbali. Habari nyingi kuhusu madhara hutoka Kagera, ambapo ugonjwa huo umesababisha hasara kubwa na ukawa na msisimko wa juu wa katika kuchochea juhudi za utafiti na ushauri wa ugani ili kuudhibiti na kusimamia kuzuka.
USIMAMIZI (MANAGEMENT)
KINGA – mambo ya kufanya kabla dalili kuonekana
- Mbinu za kitamaduni: (Cultural practices)
Ugonjwa wa BXW huenea kwa njia ya machipukizi ya kupanda, na wadudu ambao huingiza bakteria kupitia maua ya mgomba. Bakteria pia wanaweza kusafirishwa kwenye zana za kukatia. Aina zote za migomba hushambuliwa ingawa ni vigumu kwa bakteria kuambukiza baadhi ya aina mashambani kwa sababu ya hali zao za maua. Aina hizi pia zinaweza kuambukizwa kwa kupitia zana za kukatia ambazo zimebeba bakteria.
- Njia muhimu kwa mafanikio ya usimamizi ni uteuzi makini wa machipukizi yasiyokuwa na ugonjwa na kuweka zana za kutumika kwa ajili ya kukata mikungu ya ndizi na majani kuwa safi na zisizo na bakteria.
- Chagua kwa makini machipukizi ya kupanda kutoka maeneo ambapo ugonjwa huo hauko. Pata machipukizi kutoka kwa vyanzo vya kuaminika. Usitumie machipukizi kutoka kwa mimea iliyoathiriwa na BXW, hata kama machipukizi yataonekana kuwa yenye afya.
- Kuondolewa kwa ua dume kwa kutumia mkono au mti panda (ili kupunguza hatari ya kuhamisha bakteria kupitia zana za kukata) kutapunguza athari ya kuambukizwa kupitia wadudu wanaobeba mbelewele na utomvu ambao awali wamezichukua kutoka kwa mimea iliyoambukizwa. Majira ya kuyaondoa ni muhimu; maua dume yanastahili kukatwa haraka baada ya chana ya mwisho. Shida ya njia hii ni kwamba huchukua muda mwingi na baadhi ya wakulima wanaamini kuwa ua dume ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji wa juisi nzuri katika aina ya ndizi za kutengeza bia.
- Mbinu za kikemikali:
Vifaa vya kukata vinaweza kusafishwa kwa kutumia dawa ya jik (sehemu moja ya dawa na sehemu nne za maji), dawa za mimea ya kienyeji zenye uwezo wa kuua bacteria, kama vile tumbaku au pilipili, au kwa kupitisha kwenye moto. Jik ni njia ya ufanisi zaidi kwa kuua bakteria ingawa wakulima wachache huonekana kutumia njia hii.
UDHIBITI – mambo ya kufanya baada ya dalili kuonekana
- Mbinu za kitamaduni (cultural practices)
Ushauri wa awali wakati BXW ilipogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uganda ulikuwa ni kuchimba na kuchoma koo zima la mgomba. Sasa tunajua kwamba bakteria hawavamii kabisa mmea wote.Ushauri sasa hivi kwa hivyo, ni kung’oa mashina yanayoonyesha dalili ya BXW na kuyatupa kwa makini. Kutoa shina moja kutapunguza kiasi cha bakteria wanaoweza kuambukiza mimea mipya, lakini hii haitaondoa kabisa ugonjwa. Kuchagua vipandikizi vyenye afya na kusafisha vifaa vya kufanyia kazi ndio ushauri mhimu wa kufuata uliobaki.
- Mbinu za kikemikali: Mmea unapoambukizwa, hakuna tiba ya kudhibiti ugonjwa huo.
Ndugu yangu mkulima hivi ndivyo ugonjwa huu wa mnyauko ulivyo hatari, yaani ukishavamia shambani kwako njia pekee ni kung'oa migomba na kuichoma ama kuizika kabisa. Vipi uliwahi kupatwa na balaa hili? Au kuna njia ulishawahi kuitumia ulipokumbwa na ugonjwa huu ikakusaidia? Tafadhali share na sisi kwa ku-comment hapa chini.
Comments
Post a Comment