Kilimo bora cha Migomba - Part 3



kukusanya-mikungu-ya-ndizi-baada-ya-kuvuna

UVUNAJI

Zao la ndizi huweza kuanza kuvunwa katika kipindi cha miezi 9 hadi miezi 15 tangu kupandwa kwa chipukizi. Muda wa kuvunwa hutegemea hali ya hewa. Katika sehemu za joto ndizi huvunwa mapema zaidi kuliko sehemu za baridi. Pia migomba iliyopandwa kwa kutumia machipukizi huzaa mapema kuliko iliyopandwa miche iliyozalishwa kwa chupa (tissue culture).

MATUMIZI YA RIBONI

Riboni za rangi moja (au alama ya kamba) hufungwa kwenye migomba ya umri mmoja mara tu inapoanza kuchanua, na riboni ya rangi nyingine hufungwa kwenye migomba itakayoanza kuchanua wiki mbili hivi zinazofuata na kuendelea hivyo ili kurahisisha kuitambulisha mikungu ambayo itavunwa kwa wakati mmoja. Pia matumizi ya riboni hurahisiha utunzaji wa kumbukumbu ili kujua ni lini na ni mikungu mingai itavunwa.

WAKATI UNAOFAA KUVUNA

Mkungu wa ndizi huweza kuvunwa katika hatua tofauti kulingana na matumizi, aina na mahitaji ya soko. Mkungu huachwa kwenye mgomba mpaka vidole (matunda ) vimejaa. Uzito wa mkungu hongezeka haraka katika wiki mbili za mwisho, ambapo migongo ya ndizi hutoweka. Ndizi zinaweza kuvunwa zikiwa zimekomaa na zimeiva kwa kiasi cha asilimia 75 kwa ajili ya kusafirishwa mbali, pia zinaweza kuvunwa zikiwa kukomaa na zimeanza kuiva kwa ajili ya soko la karibu, au zikiwa zimekomaa na kuiva kabisa kwa ajili ya soko na matumizi ya nyumbani. Njia bora ya kukata mkungu, ni ile inayohakikisha kuwa mkungu wa ndizi hauanguki chini na kuvunja, kuchubua au kuharibu ndizi, jambo ambalo litapunguza ubora. Ukichelewa kuvuna ndizi zinaweza kuharibiwa na ndege, wanyama, wadudu au kuibiwa.
Mikungu-ya-ndizi-tayari-kwa-kunwa
Mkungu uliotayari kuvunwa
  

UBORA WA NDIZI

Ndizi zenye sifa nzuri sokoni ni zile ambazo zimekomaa kwa kiasi kinachotakiwa na zenye vidole vyenye urefu mzuri na visivyo na michubuko. Pia ziwe hazijashambuliwa na magonjwa wala wadudu waharibifu.

KIASI CHA MAVUNO

Mavuno ya ndizi hutegemea zaidi aina ya migomba, hali ya hewa, utunzaji wa mimea shambani. Mavuno huweza kufikia hadi tani 60 au zaidi kwa hekta kwa mwaka. Hata hivyo mavuno mazuri kwa mkulima wa kawaida yasipungue kati ya tani 20 hadi 30 kwa hekta kwa mwaka.
Mikungu-ya-ndizi-iliyovunwa
Mikungu ya ndizi iliyovunwa

MAGONJWA

Ugonjwa wa hatari sana ulioingia hivi karibuni katika wilaya ya Muleba na maeneo mengine mkoani Kagera kutoka nchi jirani ya Uganda ni wa Mnyauko wa migombaunaosababishwa na bakteria (Banana Bacterial Wilt). Magonjwa mengine yanayosumbua zao hili ni Kuoza tunguu, Ugonjwa wa panama, Ugonjwa wa majivu nchani mwa tunda, Sigatoka, na Moko.

WADUDU WAHARIBIFU
Wadudu wanaosumbua zaidi hili ni Minyoo fundo (Banana nematodes), na Vifukuzi (Banana weevils).

banana-weevil
Banana weevil
Banana-nematode
Banana nematode











UDHIBITI WA MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU

Magonjwa na wadudu hawa huweza kuepukwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hili. kama usafi wa shamba na kuchagua chipukizi bora. Au kupanda miche iliyozalishwa kwa chupa (Tissue culture banana seedlings) Hata hivyo mara mataizo haya yakitokea muone mtaalam wa kilimo aliye karibu ili aweze kukupa ushauri.
majani-ya-mgomba-yaliyokauka-kutokana-na-mnyauko
Migomba iliyoathiriwa na mnyauko wa migomba

Dalili nyigine za ugonjwa wa mnyauko wa migomba unaosababishwa na bakteria.
shina-la-mgomba-likitoa-utomvu-mzito
Shina la mgomba likitoa ute mzito
Ndizi-zenye-rangi-ya-kutu-kuoza
Ndizi zenye rangi ya kuoza

Ugonjwa wa mnyauko wa migomba ni ugonjwa hatar sana, umeua migomba mingi sana mkoani kagera tangu ulipoingia kwa mara ya kwanza. Huu ugonjwa ndio uliwafanya ndugu zetu Wahaya waache kutegemea ndizi kama zao lao kuu, na hivyo kuanza kulima mazao mengine ya chakula. Endelea kuusoma hapa...

Uliikosa sehemu ya kwanza au ya pili? Soma hapa Sehemu ya Kwanza      Soma hapa Sehemu ya Pili

Comments

Related posts